Posts

UTAMU NA FURAHA YA MAPENZI!

Image
       HUDUMA YA MAPENZI MATAMU! Hisia ni mawasiliano! Mapenzi ni hisia! Mapenzi ni mawasiliano! Mawasiliano matamu hutia radha katika mapenzi! Uchawi wa mapenzi upo katika mawasiliano! Kila siku tunapaswa kuwa wapya katika mahusiano yetu kwa kutafta namna tamu za kuwasiliana na wapendwa wetu katika kufikisha hisia zetu juu yao! Kwa mtu sahihi hauna haja ya kutafuta namna mpya za kumvutia!  Uwepo wako kwake ni faraja tosha ya maisha! Chamsingi usiwe mbali ya mboni zake! Hisia zinaumiza sana usipojua namna bora na njema ya kuishi maisha yako ya amani na furaha! Tumaini lako daima liwe kwa Mungu, mwanadamu tumia akili na utashi huna haja ya kujitesa hisia! AMEN! 

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MCHUMBA BORA WA MAISHA!

Image
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MCHUMBA ALIYE SAHIHI WA MAISHA! Changamoto ni kwamba katika kumpata mchumba wa maisha huwa tunayapa matamanio yetu kipaumbele cha kwanza. Baadae tunaanza kuteseka na kuhangaika katika mahusiano hayo, ambayo tunakuwa tumeyajenga juu ya vionjo vyetu vya hisia! Njia rahisi na sahihi ya kufurahia maisha ya mahusiano katika ndoa ni kumtanguliza Mungu katika kumpata mchumba wako! Tunapaswa kuhakikisha kila siku hatuchoki katika kumuomba Mungu na kumtumikia bila mawaa. Kwenye sala zetu za kila siku, kabla na baada ya usingizi mnono, tunapaswa tuombe dua kwa Mwenyezi Mungu atuchagulie mchumba mwema wa maisha! Bila ya kutaja jina, bila ya kuvuta taswira ya picha, bila ya kuvuta muonekano wa mtu na bila ya kuongozwa kwa vionjo vya hisia za kibinadamu tumtolee Mungu maombi ya kumpata mchumba mwema na bora wa maisha!  AMEN!